Katika juhudi za kuhakikisha Neno la Mungu linafika kwa kundi lengwa kwa usahihi na ufanisi, timu ya Scripture Union mkoa wa Singida imetumia mbinu ya sinema kama chombo cha uinjilisti kufikisha ujumbe wa Injili kwa jamii ya wilaya ya Ikungi.
Kupitia njia hii bunifu, jamii imepata fursa ya kusikia Habari Njema za Mungu kwa lugha yao ya Kinyaturu, kwa namna iliyo wazi na yenye mguso, zitakazowasaidia katika kuimarisha maisha yao ya kiroho na kijamii.






