Serving Children, Young People, and Families
United Nation Rd, Plot 591, Dar Es Salaam
Tel: +255 755 026 607
Email: [email protected]
Explore our blog and resources for valuable insights, expert opinions, and up-to-date information on the latest trends in the industry.
Ni kambi maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaandaa wahitimu wa Kidato cha Sita kuelekea hatua mpya ya maisha. Kupitia mafundisho mbalimbali, vijana watajengwa kiroho, kimaadili, kielimu, na kijamii ili waweze kukabiliana na maisha ya chuo na changamoto za baadaye kwa ujasiri, uadilifu, na malengo sahihi maishani.
Ni kambi maalum iliyoandaliwa kwa watoto wenye umri wa miaka 5–15 kwa lengo la kuwajenga kiroho, kimaadili, na kijamii kupitia mafundisho yenye kuwasaidia kukua katika tabia njema, nidhamu, ukweli, na ufaulu wa masomo. Kambi hii huwapa watoto nafasi ya kujifunza, kushirikiana, na kuandaliwa kuwa na maisha yenye msingi bora kwa ajili ya kesho yao.
As Scripture Union Tanzania, we extend our best wishes to all Form Six students.
Walimu kutoka Scripture Union Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika Shule ya Msingi Magufuli wakitoa mafunzo ya somo la Uinjilisti kwa wanafunzi.
Scripture Union Tanzania kwa kushirikiana na Talking Bibles International , American Bible Society, Bible Society of Kenya na Tanzania Bible Society, wamefanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Mashuleni (School Program) katika mkoa wa Singida. Mpango huu unahusisha utoaji wa mafunzo kwa walimu wa somo la dini mashuleni pamoja na ugawaji wa vifaa vya kujifunzia, ikiwemo Biblia tatu za kusoma na Biblia tatu za kuandika kwa kila shule. Lengo kuu ni kuhakikisha Neno la Mungu linawafikia wanafunzi kwa ufanisi na kuchangia katika kurejesha na kuimarisha maadili mema shuleni. Programu hii imeleta matokeo chanya miongoni mwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uelewa wa Neno la Mungu, kuimarika kwa nidhamu, na mabadiliko mazuri ya kitabia.
Kupitia njia hii bunifu, jamii imepata fursa ya kusikia Habari Njema za Mungu kwa lugha yao ya Kinyaturu,
For 8 years, Sister Magret has walked faithfully with Scripture union Tanzania (SUT), Becoming a pillar of prayer, encouragement and inspiration in youth ministry.
Kupitia mafunzo ya walimu wa dini yaliyofanyika Singida na Tabora, mpango huu unasaidia kujenga maadili mema, kuimarisha msingi wa kiroho, na kuhusisha makanisa katika jamii. Lengo kuu ni kukuza kizazi chenye hofu ya Mungu, maadili mema, na kinachochangia katika ujenzi wa taifa lenye uadilifu na amani.
Tarehe 5 Agosti 2025, viongozi wa makanisa walikusanyika kwa mafunzo maalum ya School Program yaliyofanywa na Scripture union of Tanzania kwa kushirikiana na Talking Bible International, mpango unaolenga kukabiliana na mporomoko wa maadili nchini kupitia kuwafikia watoto shuleni na katika jamii kwa Neno la Mungu.