Tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Mashuleni

Scripture Union Tanzania kwa kushirikiana na Talking Bibles International , American Bible Society, Bible Society of Kenya na Tanzania Bible Society, wamefanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Mashuleni (School Program) katika mkoa wa Singida. Mpango huu unahusisha utoaji wa mafunzo kwa walimu wa somo la dini mashuleni pamoja na ugawaji wa vifaa vya kujifunzia, ikiwemo Biblia tatu za kusoma na Biblia tatu za kuandika kwa kila shule. Lengo kuu ni kuhakikisha Neno la Mungu linawafikia wanafunzi kwa ufanisi na kuchangia katika kurejesha na kuimarisha maadili mema shuleni. Programu hii imeleta matokeo chanya miongoni mwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uelewa wa Neno la Mungu, kuimarika kwa nidhamu, na mabadiliko mazuri ya kitabia.

Tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Mashuleni