Walimu kutoka Scripture Union Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika Shule ya Msingi Magufuli wakitoa mafunzo ya somo la Uinjilisti kwa wanafunzi. Kufundisha Uinjilisti katika ngazi ya msingi ni muhimu sana kwa sababu ndiyo hatua ya mwanzo ya kumjenga mtoto katika msingi imara wa kiroho na kimaadili. Biblia inasema: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” (Mithali 22:6, KJV). Hii inaonesha wazi umuhimu wa kuwafundisha watoto Neno la Mungu tangu wakiwa wadogo. Hivyo, kuwafundisha watoto Uinjilisti ni kuwasaidia wamjue Mungu mapema, wakue katika maadili mema, upendo, heshima na uwajibikaji. Kupitia mafundisho haya, watoto hujifunza kuwa mashahidi wema wa Kristo katika familia, shuleni na katika jamii, na huandaliwa kuwa viongozi bora na raia wema wa baadaye.







