Mbeya, Tanzania — Tarehe 5 Agosti 2025, viongozi wa makanisa walihudhuria mafunzo ya School Program, mpango wa kimkakati uliobuniwa ili kukabiliana na ongezeko la mporomoko wa maadili nchini.
School Program inalenga kuwawezesha walimu wa dini na viongozi wa makanisa kufikisha Neno la Mungu mashuleni na katika jamii. Kupitia mafunzo haya, washiriki walifundishwa namna ya kutumia vifaa vya kufundishia kama vile Talking Bible (Biblia inayosomwa kwa sauti) na Biblia za kusoma, ili kuhakikisha watoto wanapata nafasi ya kusikia na kujifunza Neno la Mungu kwa njia mbalimbali.
Mafunzo yalihusisha pia mbinu za kuendesha vipindi vya mafundisho, namna ya kutumia vifaa husika kwa ufanisi, pamoja na taratibu za kutoa taarifa za maendeleo ya mpango.
Waandaaji wa mafunzo walisisitiza kuwa kurejesha maadili miongoni mwa vijana kunahitaji jitihada za makusudi za kuwapatia mafundisho ya Biblia kwa uwazi na kwa uendelevu. Kupitia mpango huu, watoto watajengewa misingi ya imani, nidhamu na heshima, hivyo kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kwa jitihada hizi, School Program inalenga kulea kizazi chenye maadili na kinachoongozwa na misingi ya Neno la Mungu, ili kukabiliana na changamoto za kimaadili zinazoikumba taifa kwa sasa.

.jpeg%3F_a%3DBAMABkiu0&w=3840&q=75)
.jpeg%3F_a%3DBAMABkiu0&w=3840&q=75)








